Amos 2:1-3

1 aHili ndilo asemalo Bwana: “Kwa dhambi tatu za Moabu,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu,
ikawa kama chokaa.

2 bNitatuma moto juu ya Moabu
ambao utateketeza ngome za Keriothi.
Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa
katikati ya vilio vya vita na mlio wa tarumbeta.

3 cNitamwangamiza mtawala wake
na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,”
asema Bwana.

Copyright information for SwhKC